Rais Dkt. Mwinyi Azungumza na Uongozi wa Chuo cha Msolopa
Sep 24, 2024
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na ujumbe wa uongozi wa Chuo cha Msolopa Kilimani “Al Madrasatul Swiffati Nnabawiyyatil Karimah” mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 24-9-2024, walipofika kwa mazungumzo na kujitambulisha, (kulia kwa Rais) Sheikh.Sayyid Othman Abdulqadir Othman Mlezi wa Zawiyyatul Qadiria Tanzania, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali,
Na
Ikulu - Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu kinachoelezea “Ndoa na Talaka katika Sheria ya Kiislamu” akikabidhiwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, baada ya kumaliza mazungumzo na Uongozi wa “Al Madrasatul Swiffati Nnabawiyyatil Karimah” (Msolopa Kilimani) yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo 24-9-2024.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Sheikh Sayyid Othman Abdulqadir Othman, Mlezi wa Zawiyyatul Qadiria Tanzania, baada ya kumaliza mazungumzo na uongozi wa Chuo cha Msolopa Kilimani “Al Madrasatul Swiffati Nnabawiyyatil Karimah”, yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo 24-9-2024.