Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Apokea Salamu za Pole Kutoka Kwa Viongozi Mbalimbali Ikulu Migombani
Mar 06, 2024
Rais Dkt. Mwinyi Apokea Salamu za Pole Kutoka Kwa Viongozi Mbalimbali Ikulu Migombani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakizungumza na viongozi wa Vyama Rafiki (9) vya Siasa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Ndg. Ameir Hassan Ameir, (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu Migombani kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa kufiwa na Baba yake Mzazi Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Na Ikulu - Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko alipofika Ikulu Migombani jijini Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa Mhe. Rais kwa kufiwa na Baba yake Mzazi Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi  wakizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi alipofika Ikulu Migombani jijini Zanzibar kwa ajili ya kuhani na kutoa mkono wa pole kwa Rais wa Zanzibar baada ya kufiwa na baba yake Mzazi Rais Mstaafu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi  wakizungumza na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipofika Ikulu Migombani jijini Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa Mhe. Rais kwa kufiwa na baba yake mzazi Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu wa Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijiji kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akiongoza Ujumbe wa Viongozi wa SMZ walipofika Ikulu Migombani jijini Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa Mhe. Rais, kwa kufiwa na Baba yake Mzazi  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi , aliyefarika wiki iliyopita na kuzikwa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa akiongoza Ujumbe wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ya Unguja na Pemba walipofika Ikulu Migombani jijini Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa Mhe. Rais kwa kufiwa na Baba yake Mzazi Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi