Rais Dkt. Mwinyi Akabidhiwa Ripoti ya Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa
Oct 10, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum (Kikosi Kazi) ya Kuchangia maoni ya washiriki wa mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo tarehe 10/10/2022.
Wajumbe wa Kamati Maalum (Kikosi Kazi) ya Kuchangia maoni ya washiriki wa mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar katika hafla ya kukabidhi ripoti ya mkutano wa Wadau hao uliofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti Kamati Maalum (kikosi Kazi), Dkt.Ali Uki, ripoti ya Wajumbe wa Kamati Maalum (Kikosi Kazi) ya Kuchangia maoni ya washiriki wa mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, kwa ajili ya kuifanyia kazi katika hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar tarehe 10/10/2022.