Rais Dkt. Mwinyi Akabidhi Boti kwa Wavuvi na Wakulima wa Mwani Tumbe na Kulifungua Soko la Samaki
Jul 27, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyiakizungumza na Wananchi wa Tumbe wakati wa hafla ya kukabidhi Boti kwa Wavuvi wa Samaki na Wakulima wa Mwani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo leo 26-7-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kulifungua Soko la Samaki Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba leo 26-7-2022, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyiakimkabidhi Boti ya Uvuvi Kiongozi, Ndg. Faki Mpemba Faki kwa ajili ya Uvuvi wa Samaki, hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Soko la Samaki Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba.