Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Afungua Viwanja vya Matumbaku Sports Complex
Dec 30, 2023
Rais Dkt. Mwinyi Afungua Viwanja vya Matumbaku Sports Complex
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (wa nne kulia) na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum wakifungua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Viwanja vya Matumbaku Sports Komplex Miembeni leo ,Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi katika maadhimisho ya shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe  kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Viwanja vya Matumbaku Sports Komplex Miembeni, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika maadhimisho ya shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Juma Akili Malik, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Mohamed (Dimwa), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF), Ndg,Nassor Shaaban Ameir.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa funguo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita katika hafla ya  ufunguzi rasmi wa Viwanja vya Matumbaku Sports Komplex Miembeni ,Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika maadhimisho ya shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) Ndg, Nassor Shaaban Ameir na kushoto nWaziri wa Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum. 

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi kikombe Nahodha wa Timu ya   Karume Boys, Ashraf Ali Othman, baada ya ushindi na Timu ya ZSSF katika mchezo wa Ufunguzi wa Vyanja vya Matumbaku Sports Komplex Miembeni  Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika maadhimisho ya shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF), Ndg. Nassor Shaaban Ameir .

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Timu ya   Karume Boys baada ya ushindi wa bao 1-0  na Timu ya ZSSF katika mchezo wa Ufunguzi wa Vyanja vya Matumbaku Sports Komplex Miembeni  Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika maadhimisho ya shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipuliza filimbi kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Kiwanja cha Mipira cha Matumbaku wakati wa Ufunguzi rasmi wa Viwanja vya Matumbaku Sports Komplex Miembeni, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika maadhimisho ya shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kulia) Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum, (wa pili kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi  (kushoto)  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF), Ndg,Nassor Shaaban Ameir.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za ufunguzi rasmi wa Viwanja vya Matumbaku Sports Komplex Miembeni ,Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika maadhimisho ya shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mgeni rasmi alikuwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi