Rais Dkt. Mwinyi Afungua Mkutano Mkuu wa 44 wa Umoja wa Wanabima Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika
Aug 29, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
MwenyekitiI wa Bodi ya Umoja wa Makampuni ya Bima Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi.Patty Karuaihe Martin akitoa maelezo ya Umoja huo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 44 wa Umoja wa Wanabima Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika uliyofanyika leo 29-8-2022, katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Unguja Jijini Zanzibar na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masawara Group, Bw. Shingai Mutasa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 44 wa Umoja wa Wanabima Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 29-8-2022, uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum akizungumza wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 44 wa Umoja wa Wanabima Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Wilaya ya Magharibi “B”Unguja Jijini Zanzibar leo.29-8-2022.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 44 wa Umoja wa Mashirika ya Bima, Ukanda wa Mashariki na Kusini Mwa Afrika wakifuatilia kwa makini hotuba iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Madinat Al Bahr Hotel.