Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Mafuguli: Viongozi na Watendaji Msisubiri Maelekezo ya Rais Kutimiza Wajibu Wenu
Jul 03, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33229" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Immaculate Makilika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka viongozi na watendaji wa serikali kuuacha kusibiri  maelekezo ya viongozi wakuu wa kitaifa katika kutekeleza majukumu katika maeneo yao ya kazi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uapisho wa Viongozi na Watendaji 16 wa Serikali Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo aliwataka viongozi na watendaji hao kutekeleza vyema wajibu wao katika kuwaletea maendeleo wananchi

[caption id="attachment_33230" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

“Nasikitika pale ambapo viongozi wa serikali kama vile  kama mawaziri, naibu waziri hata wakurugenzi wanashindwa kutoa matamko na kutafutia ufumbuzi matatizo ya wananchi, ninataka mkafanye kazi katika maeneo yenu na si kusubiri mimi, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu tutoe matamko” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alielezea sababu mbalimbali zilizosababisha kufanya mabadiliko hayo katika Baraza lake la Mawaziri, ambazo ni kutoridhishwa na utendaji kazi katika baadhi ya Wizara ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo aliutaja Mkataba baina ya Wizara hiyo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kupitia mradi wa mashine za utambuzi wa alama za vidole  katika vituo 108 vya Polisi uliogharibu Tsh. Bilioni 37.

Aidha Rais Magufuli pia aliieleza suala lingine ni pamoja na Mradi wa magari 777 yaliyoagizwa na Wizara hiyo kwa kutumia mkataba usio na maslahi na nchi, ambapo kati ya magari hayo, baadhi yake yalionekana kutumika kwa zaidi ya kilometa 4000, mengine kutoonesha  mwaka ambao magari hayo yalitengenezwa.

[caption id="attachment_33231" align="aligncenter" width="750"] Kangi Lugola akila Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_33232" align="aligncenter" width="750"] Viongozi mbalimbali walioapishwa wakila Kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

“changamoto nyingine kuwa ni kuwepo kwa sare hewa za askari, upotevu wa mabilioni ya fedha, Jeshi la zima Moto na Uokoaji kutokuwa na vitendea kazi vya kutosha ambapo nimeelezwa jeshi hili lina magari 53 pekee na utoaji wa kiholela wa vibali vya wageni kufanyakazi nchini” alisema Rais Magufuli..

Aidha, akizungumzia kuhusu sekta ya maji, Rais Magufuli alimwagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa kukamilisha miradi mbalimbali ya maji ili kutatua kero ya muda mrefu inayowakabili Watanzania hususani wa maeneo ya vijijini

Aliongeza kuwa hivi karibuni Serikali ilipokea kiasi cha Tsh trilioni 1.2 kutoka nchini India kwa ajili ya kugharamia shughuli za usambazaji wa maji katika mikoa 17 nchini, hivyo ni wajibu wa Wizara ya  Maji na Umwagiliaji ijipange katika kuhakikisha kuwa miradi hiyo inatekelezwa bila kuwa na ucheleweshwaji.

[caption id="attachment_33233" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_33235" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Moses Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Picha na Ikulu[/caption]

Naye Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa alisisitiza kuwa Wizara yake itahakikisha kuwa itasimamia vyema wajibu na majukumu yake katika kuwahudumia Wananchi kwa kuwa kuna fedha za kutosha za zilizotengwa na Serikali katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Rais John Magufuli amewapisha viongozi mbalimbali wakiwemo  Mawaziri, Naibu Waziri, Katibu Wakuu, Naibu Katibu Wakuu, Mwenyekiti, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Makamu Mwenyekiti, Makamishana, pamoja na Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi