Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Magufuli Asajili Laini ya Simu, Atoa Pole kwa Familia ya Bw. Atanasi Mnaku
Dec 27, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_49930" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafamilia pamoja na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao leo Disemba 27, 2019.[/caption] [caption id="attachment_49937" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka alama ya kidole gumba alipokwenda kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole katika kampuni ya simu ya Airtel Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.Kushoto ni Msajili wa laini za Simu wa Airtel tawi la Chato Michael Martin.[/caption]

Mhe. Rais Magufuli amefanya usajili huo Chato Mjini katika Mkoa wa Geita.

Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia tarehe 01 Januari, 2020 hadi tarehe 20 Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA kutokana sababu mbalimbali zikiwemo kuugua na kukamilisha upataji wa namba ama Vitambulisho vya Taifa.

Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya muda huo hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa

[caption id="attachment_49934" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27,2019.[/caption] [caption id="attachment_49936" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho chake cha Taifa Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin aliokwenda kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.[/caption] [caption id="attachment_49939" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha simu yake ambayo ametoka kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kisha kuzungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote ambapo ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.[/caption] [caption id="attachment_49940" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.[/caption] [caption id="attachment_49942" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mjasiliamali wa Chipsi Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.[/caption]

Amefafanua kuwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi ikiwemo kuepusha vitendo vya utapeli na ujambazi vinavyofanywa na wahalifu, ambao licha ya wengi wao kukamatwa na vyombo vya dola wameendelea kusababisha usumbufu na upotevu mali za wananchi hususani fedha.

Pamoja na kuwasalimu wananchi wa Chato Mjini waliojitokeza kushuhudia wakati akisajili laini yake kwa alama za vidole, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu na kusikiliza maoni yao kuhusu zoezi hili na pia mwananchi Steven Joseph Wandwi anayefanya biashara ya kuuza chipsi na mishikaki akawaongoza wenzake kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kumshukuru kwa utumishi wake mzuri ulioongeza kasi ya maendeleo kwa Taifa hasa vijana ambao sasa wanachapa kazi bila bughudha.

Kabla ya kwenda kusajili laini yake ya simu, Mhe. Rais Magufuli ametembelea Mtaa wa Chato Kati na ametoa pole kwa familia ya Marehemu Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki dunia juzi tarehe 25 Desemba, 2019 na mazishi yake yamepangwa kufanyika kesho.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato

27 Desemba, 2019

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi