Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Afungua Barabara ya Bagamoyo—Makofia- Msata yenye Urefu wa Kilometa 64.
Jun 22, 2017
Na Msemaji Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa Kiserikali na Wabunge, akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Pwani na Dar es Salaam mara baada ya kufungua barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata yenye urefu wa kilometa 64. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Mama Salama Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kiwangwa wakati akielekea kufungua barabara ya bagamoyo-Msata mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akielezea hatua za ujenzi wa Madaraja katika barabara ya Bagamoyo-Msata huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi