Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Pwani, Simiyu na Singida Zaendelea Kufanya Vizuri UMISSETA
Jun 20, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Mikoa ya Pwani, Simiyu, na Singida ndiyo inayoonekana kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya UMISSETA yanayotarajiwa kukamilika tarehe 21 juni 2019. Mkoa wa Pwani umepata medali 7 za dhahabu, 1 ya fedha na 2 za shaba, na hivyo kujipatia jumla ya medali 10 kwenye mashindano hayo. Simiyu imepata medali 2 za dhahabu, 5 za fedha na 2 za shaba jumla ina medali 9 Mkoa wa Singida nao haukuwa nyuma katika kupata medali ambapo walipata medali 3 za dhahabu, 5 za fedha na 3 za shaba, hivyo jumla wamepata medali 11. Mkoa wa Mwanza nao haukuwa nyuma katika kupata medali ambapo walifanikiwa kupata medali 3 za dhahabu, huku jirani zao shinyanga wakipa media 1 ya dhahabu, 1 ya fedha na 2 za shaba. Mkoa wa Geita nao ulipata media 1 ya dhahabu, wakati Tabora wao walipata media 1 ya dhahabu, 3 za fedha na 1 ya shaba, na Manyara wamepata medali 2 za fedha na 5 za shaba, huku wenzao wa Arusha wamepata medali 2 za dhahabu 1 ya fedha. Mkoa wa Unguja nao haukuwa nyuma katika ushindi wa medali mwaka huu ambapo walijinyakulia medali 3 za dhahabu, 1 ya fedha na 1 ya shaba. Mikoa mingine ambayo haikutoka kapa ni pamoja na Dar es salaam ambao wamepata medali 3 za dhahabu, 1 ya fedha na 1 ya shaba, mkosa wa Lindi nao ulipata medali moja ya fedha huku mikoa mingine 11 ikiambulia patupu. Mikoa iliyokosa kabisa medali katika mashindano ya riadha mwaka huu ni pamoja na Katavi, Ruvuma, Tanga, Pemba, Mtwara, Njombe, na Rukwa. Mikoa mingine ni pamoja na Iringa, Kagera Songwe  na Morogoro.  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi