Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

PS3 Kuchochea Mageuzi Katika Kuandaa Bajeti na Mipango ya Serikali
Jul 24, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Elias Nyabusami akifungua mafunzo yaWaganga Wakuu, Makatibu wa Afya,Maafisa TEHAMA,Maafisa Mipango,Wahasibu na Wachumi kutoka katika Mikoa ya Lindi,Mtwara, Ruvuma na Dar es Salaam kuhusu mfumo mpya wa kuandaa Mipango na bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo mjini Mtwara.[/caption]  

[caption id="attachment_7342" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha Kutoka mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama (Public Sector Systems Streghthen PS3.) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) Bw. Gemini Mtei akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo Mjini Mtwara.[/caption]

Frank Mvungi-Mtwara

Serikali itaokoa Kiasi Kikubwa cha Fedha kutokana na kuanza kutumika kwa mfumo ulioboreshwa katika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa uitwao Plan Rep unaoenda sambamba na mafunzo yanayoendeshwa kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama (Public Sector Systems Streghthen PS3.) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Akifungua mafunzo kwa Waganga Wakuu, Makatibu wa Afya, Maafisa TEHAMA, Maafisa  Mipango, Wahasibu,  na Wachumi kutoka katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Dar es Salaam, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw.Elias Nyabusami amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka na yatasaidia kuondoa Changamoto zilizokuwa zikijitokeza kabla ya kuwepo kwa mfumo huo.

‘’Kutokana na mabadiliko na kurahisishwa kwa Teknolojia mfumo mpya wa Plan Rep umerahisihwa kwa kufanywa kuwa web Based na utawezesha Halmashauri kuingiza taarifa za mipango na bajeti moja kwa moja kwa njia ya mtandao na kuweza kutumwa kwenye mfumo mmoja uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kufanyiwa kazi na kuingizwa kwenye bajeti Kuu ya mwaka husika”Alisisitiza Nyabusami

Akifafanua amesema kuwa mfumo huo utasaidia kutoa mrejesho wa mara kwa mara kwa ngazi husika za utawala kwa wakati na hakutakuwa tena na haja ya wahusika kusafiri  kutoka katika vituo vyao vya kazi ili kushughulikia masuala ya bajeti na Mipango kwa kuwa sasa yatafanyika katika Mikoa na Halmashauri husika.

[caption id="attachment_7343" align="aligncenter" width="750"] Afisa TEHAMA mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Archibold Kundasai akitoa maelezo kwa washiriki kuhusu faida za mfumo wa PS3 wakati wa hafla yaufunguzi wa mafunzo hayo.[/caption]

Kwa upande wake Mkuu wa timu ya Rasilimali Fedha Kutoka mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama (Public Sector Systems Streghthen PS3.)  Bw. Germini Mtei amesema kuwa kupitia mfumo mpya wa Plan Rep Mipango yote na Bajeti za Vituo vya kutolea Huduma kwa wananchi itaonekana kupitia mfumo huo hali itakayosaidia kuongeza ufanisi, uwazi, uwajibikaji na kuboreshwa kwa utoaji huduma.

“Kwa kutumia mfumo huu mpya sasa tunaamini kuwa utasaidia kuondoa ucheleweshaji wa fedha kwenda kwenye miradi na upotevu wa fedha kwa kuwa kila kitu kitafanyika kwa njia ya mtandao” Alisisitiza Bw.Mtei.

Aliongeza kuwa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za Umma (PS3) unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara na PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ikiwemo kuimarisha mifumo ya mawasiliano,Utawala Bora,Fedha na rasilimali watu,husasani kwa jamii zenye uhitaji.

[caption id="attachment_7354" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Elias Nyabusami (Katikati) akiwa na sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo hayo.[/caption]

Aidha Afisa TEHAMA mwandamizi toka Ofis ya Rais TAMISEMI Bw. Archibold Kundasai amesema kuwa mipango yote kuanzia ngazi ya Kata,Halmashauri na Mikoa itakuwa katika mfumo huo na dhamira ya Serikali ni kuongeza tija katika kuwahudumia Wananchi.

“Bajeti ilikuwa ikichukua muda mrefu kuandaliwa ambapo takribani miezi 4 ilitumika ambapo kwa mfumo huu tija itaongezeka kwa kuwa wahusika watabaki katika vituo vyao wakihudumia wananchi huku wakitekeleza jukumu la Kuandaa Bajeti na Mipango yao” Alisisitiza Kundasai

Naye Mshiriki wa Mafunzo hayo Bw. Ezekiel Buyagaza ambaye ni Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi amesema kuwa anaipongeza Serikali kwa maboresho yanayofanyika hali itakayochochea tija katika kutoa huduma kwa wananchi.

Serikali ya Tanzania na USAID kupitia mradi wa uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) imeandaa mafunzo haya kwa watumiaji wake nchi nzima,Mafunzo yanatolewa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Wakala ya Serikali mtandao,Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora,Wizara ya Fedha na Mipango,Wizara ya afya na unatarajiwa kutumiwa na watumiaji 1500 watakaofundishwa matumizi ya mfumo huo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi