[caption id="attachment_8923" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kutoka Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wakiteta jambo wakati wa semina kuhusu Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) inayoendelea Jijini Mbeya leo . Semina hiyo imewakutanisha Maafisa Mipango wa Wilaya, Waganga Wakuu, Makatibu Afya wa Mikoa na Wilaya, Wawekahazina, na Maafisa Tehama kutoka Halmashauri za Mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe na wenyeji Mbeya.[/caption]
Na: Frank Shija – MAELEZO, Mbeya
Mfumo huu ulioboreshwa umekuja wakati muafaka ambapo utaongeza ufanisi na uwajibikaji katika utendaji kazi wakati wa kuandaa mipango na bajeti hadi katika utekelezaji wake.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Bw. Ambwene Isaya alipozungumza na mwandishi wa Habari hizi katika semina kuhusu Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) kwa watumiaji wa mfumo huo inayoendelea Jijini Mbeya.
Amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa utaratibu mzuri wa utendaji kazikupitia mfumo huo kila mhusika atawajibika kwa wakati jambo ambalo litarahisisha utekelezaji wa majukumu na utoaji wa huduma kwa wananchi.
[caption id="attachment_8929" align="aligncenter" width="750"] Msahuri wa Masuala ya Fedha kutoka Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bi. Hellen Nyagwa akisisitiza jambo wakati wa semina kuhusu Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) inayoendelea Jijini Mbeya. Semina hiyo imewakutanisha Maafisa Mipango wa Wilaya, Waganga Wakuu, Makatibu Afya wa Mikoa na Wilaya, Wawekahazina, na Maafisa Tehama kutoka Halmashauri za Mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe na wenyeji Mbeya.[/caption]“Sisi tunauona mfumo huu ulioboreshwa ni mfumo utakaotusaidia sana katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yetu katika kila ngazi ya utekelezaji, ” alisema Isaya.
Akizungumzia changamoto watakazokabiliana nazo amesema kuwa kutokana na mfumo huu kufanyakazi kwa uwepo wa mtandao, ikitokea mtandao huko chini kazi zitasimama lakini pia mfumo huu utawalazimu watumiaji kufahamu matumizi ya Kompyuta kwa ufasaha jambo ambalo wengine itakuwa changamoto kwao kutokana na kutopenda kwenda na wakati.
Akitoa ulinganifu kati ya mfumo wa awali na huu ulioboreshwa Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Adam Msumule amesema kuwa mfumo wa zamani ulikuwa hautoi fursa ya mtumiaji kufanya kazi akiwa mbali na Kompyuta iliyowekwa program maalum jambo ambalo kwa sasa mfumo umerahishwa kwa kuwa utakuwa ni kwa njia ya mtandao ambapo mtu ataweza kufanya kazi yake akiwa mahali popote.
[caption id="attachment_8930" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Timu ya Wawezeshaji Kitaifa wa Mfumo wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti Katika Serikali za Mitaa (PlanRep) Bw. Frank Makua Charles akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu Mfumo huo inayoendelea Jijini Mbeya leo . Semina hiyo imewakutanisha Maafisa Mipango wa Wilaya, Waganga Wakuu, Makatibu Afya wa Mikoa na Wilaya, Wawekahazina, na Maafisa Tehama kutoka Halmashauri za Mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe na wenyeji Mbeya.[/caption] [caption id="attachment_8931" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa semina kuhusu Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia kwa makini katika kupitia Kompyuta zao namna mfumo huo unavyofanya kazi wakati wa semina hiyo inayoendelea Jijini Mbeya leo . Semina hiyo imewakutanisha Maafisa Mipango wa Wilaya, Waganga Wakuu, Makatibu Afya wa Mikoa na Wilaya, Wawekahazina, na Maafisa Tehama kutoka Halmashauri za Mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe na wenyeji Mbeya.[/caption]Aliongeza kuwa kupitia mfumo huu suala zima la uwazi na uwajibikaji litaongezeka kutokana na kila muhusika atapaswa kutekeleza wajibu wake ipasavyo na kwa wakati kwa kuwa mfumo umetengenezwa kwa namna ambayo mtu anaweza kujifanyia tathmini ya utendaji wake.
“Kupitia mfumo huu mpya itakuwa rahisi sana kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na matumizi ya fedha zilizoidhinishwa katika miradi husika kwakuwa kutakuwepo na muingiliano na mifumo mingine kama ule wa Epicar tofauti na mfumo wa zamani, ” alifafanua Msumule.
Kwa upande wake Mkuu wa Timu ya Fedha kutoka Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Dkt. Gemini Mtei amesema kuwa ili kuhakikisha wanakabiliana na changamoto ya mtandao wameanza kuunganisha mfumo wa mawasiliano ya mtandao ya ndani (LAN) ambapo takribani Halmashuri 93 za Tanzania bara zimeingizwa katika mpango huo.
Dkt. Gemini amesema kuwa pamoja na changamoto hiyo PS3 imeendelea kusshirikiana na Serikali katika kuzijengea uwezo wa kimawasiliana Halmashauri nchini ambapo hadi sasa imefanikiwa kuwepo kwa mfumo wa mawasiliano ya Tovuti katika Halmashuri zote za Tanzania Bara jambo linaloongeza hamasa katika kuhakikisha kuna kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mawasiliano ya mtandao.
[caption id="attachment_8932" align="aligncenter" width="750"] Muwezeshaji wa Kitaifa wa Mfumo wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) ambaye pia ni Katibu wa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Bi. Glory Laizer akimuelekeza jambo mmoja wa washiriki wa semina kuhusu mfumo huo inayoendelea Jijini Mbeya leo. Semina hiyo imewakutanisha Maafisa Mipango wa Wilaya, Waganga Wakuu, Makatibu Afya wa Mikoa na Wilaya, Wawekahazina, na Maafisa Tehama kutoka Halmashauri za Mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe na wenyeji Mbeya.[/caption]Katika kuhakikisha watumiaji wa mfumo huu wanajengewa uwezo Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kushirikiana na USAID-Tanzania/PS3 wanaendesha mafunzo katika maeneo mabalimbali nchini kuhakikisha wanawafikia walengwa ili kujiweka tayari kwa matumizi ya mfumo huo pindi utakapozinduliwa rasmi. Mafunzo kama haya yamefanyika kikanda katika mikoa ya Mwanza na Mtwara, pia yanaendelea katika mikoa ya Kigoma, Morogoro na Mbeya.
Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) umeandaliwa na wataalamu wa Kizalendo kupitia Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID Tanzania) kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).