Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ofisi ya Waziri Mkuu Yakidhi Viwango vya Osha
Feb 02, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50625" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa[/caption]

 MAMLAKA ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imetoa cheti kwa Ofisi ya Binafsi ya Waziri Mkuu baada ya kufanyia ukaguzi katika maeneo yote ya ofisi hiyo na kuonesha kuwa  yamekidhi viwango.

 Cheti hicho kimetolewa jana jioni (Jumamosi, Februari 1, 2020) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda na kupokelewa na Katibu wa Waziri Mkuu Bw. Raymond Gowelle.

 Akikabidhi cheti hicho, Bi Khadija aliipongeza mersin escort Ofisi hiyo kwa kuonesha mfano wa uetekelezaji wa sheria, ambapo amezishauri ofisi nyingine za umma ziige.

 “Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu imeonesha mfano wa kuigwa kwa utekelezaji wa sheria, kwani walituita tukaja kufanya ukaguzi na tukatoa maelekezo ya namna ya kuboresha baadhi ya maeneo na wamerekebisha.”

 Alisema baada ya kutekeleza maelekezo hayo suala lililokuwa limebakia ni upimaji wa afya kwa wafanyakazi pamoja na kutoa mafunzo ya huduma ya kwanza ambayo yamefanyika leo (jana).

 Mtendaji huo alisema ni muhimu kwa ofisi zote kuzingatia sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.

 Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA, pia watumishi wa Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu walikumbushwa namna bora ya kufanyakazi kwa uadilifu. Mafunzo yalitolewa na watalaamu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 Watumishi hao waliushukuru uongozi wa ofisi kwa kuandaa zoezi la upimaji wa afya ambao ulikuwa na muitikio mkubwa, mafunzo ya huduma ya kwanza pamoja na kukumbushwa kuhusu uadilifu na matumizi ya porn madaraka na ofisi kwa manufaa ya umma.

IMETOLEWA NA

OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAPILI, FEBRUARI 2, 2020.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi