Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

NSSF Yaaswa Kuimarisha Mifumo ya Kielektroniki katika Ukusanyaji Mapato
Oct 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37508" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wajumbe wa Bodi ya wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa NSSF leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo leo.[/caption] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka bodi mpya ya  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kusimamia mapato kwa kutumia mifumo ya kielektroniki. Akizungumza hii leo, Jijini Dodoma Oktoba 27, 2018 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko huo, Waziri Mhagama amesema kuwa mifumo ya kielektroniki itasaidia kuimarisha makusanyo na matumizi ya fedha ndani ya shirika hilo. "Wekeni mkakati  ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato ikiwemo kuhakikisha kuwa mnaimarisha mifumo ya kielektroniki kuongeza mapato na kuongeza tija kwa kuwa mifumo hii itasaidia katika kudhibiti mapato ya mfuko," Alisisitiza Mhe. Mhagama Akifafanua mhe. Mhagama amesema kuwa sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi ambapo mpaka sasa sekta hiyo imewekeza jumla ya trilioni 11.79 katika miradi mbalimbali. Akizungumzia miradi  inayotekelezwa amesem kuwa ni pamoja na miundombinu, vifaa tiba na elimu ambayo inaleta tija katika kuchochea maendeleo ya Taifa na ustawi wa wananchi. Akizungumzia suala la ujenzi wa uchumi wa viwanda mhe. Mhagama amesema kuwa mfuko huo una jukumu la kuhakikisha kuwa miradi yote inayotekelezwa inalenga katika kuimarisha hali ya uchumi kupitia katika ujenzi wa viwanda. "Bodi hii imesheheni wataalam wanaoaminika, tunaamini wataenda kuondoa changamaoto mbalimbali zinazokabili shirika hilo," Alisisitiza Mhe. Mhagama. Akifafanua amesema kuwa Bodi hiyo inalo jukumu la kufanya usimamizi bora wa mapato ambao utaendana na utengenezaji wa mifumo bora ya kielekitroniki ili kuimarisha usimamizi wa fedha za mfuko huo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Ali Idi Siwa amesema kuwa watashirikiana na menejimenti ya mfuko huo kuhakikisha kuwa wanatimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisistiza katika kukuza uchumi kupitia ujenzi wa viwanda. Aliongeza kuwa  tayari wameshajiwekea mikakati ya utendaji wa Bodi hiyo ambapo hali hiyo itaongeza tija na kutimiza malengo kwa wakati Bodi ya NSSF imezinduliwa kisheria chini ya sheria  namba 53 ya mfuko huo ya mwaka 1997.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi