Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Nchi Haitoingia Gizani-Msigwa
Jan 31, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Daudi Manongi - PWANI


Serikali imesema kuwa nchi haitoiingia gizani kutokana na  kazi ya uboreshaji wa visima vya gesi vilivyopo Songosongo kwani ni marekebisho ya kawaida.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akitoa taarifa ya Serikali kupitia vyombo vya habari Kibaha, Pwani.

“Tangazo lililotolewa na TANESCO kuhusu zile siku kumi za kuanzia tarehe 01 Februari hadi tarehe 10 Februari za kazi ya uboreshaji wa visima vya gesi vilivyopo Songosongo hautasababisha nchi iingie gizani kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vinaripoti. Lile ni zoezi la kawaida la kuboresha mfumo na Serikali inawaomba wananchi muwe mnasikiliza matangazo ya TANESCO wenyewe ” ,amesema Msigwa.

Amesema Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha katika Gridi ya Taifa na hivyo ipo miradi mbalimbali inayotekelezwa kufanikisha mpango huu, na hasa baada ya kukutana na changamoto ya kupungua kwa maji katika vyanzo ambavyo vinazalisha umeme kwa kutumia maji.

Ameongeza kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linameanza kuchukua hatua ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi yetu ambayo tunayo hifadhi ya zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57.

Aidha, amesema kazi ya kufunga mitambo itakayozalisha megawati 112 za umeme inaendelea, tayari megawati 60 zimepatikana na kuingizwa katika Gridi ya Taifa na zilizobaki zitaingizwa katika mwezi ujao wa Februari.

“Aidha, Upanuzi wa mradi Kinyerezi II ambao utaongeza megawati 185 juu ya megawati 150 zinazozalishwa sasa unaendelea, mwezi Aprili mwaka huu megawati 70 za mwanzo zitaingizwa katika gridi hiyo na ifikapo Agosti mwaka huu 2022 megawati zote 185 zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.”amesema Msigwa

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi