Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

NBS Watakiwa Kutumia Lugha Nyepesi Katika Utoaji Takwimu
Jul 03, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33272" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), kilichofanyika leo Jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa na Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bi. Margreth Jacob.[/caption]

Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwanyika ameitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kutoa elimu ya matumizi sahihi ya takwimu ambazo zitamsaidia mwananchi wa kawaida kwenye maisha yake ya kila siku.

Bi. Dorothy ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (MST) George Mkuchika,  leo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa NBS.

[caption id="attachment_33274" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa NBS, Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.[/caption]

Amesema kuwa takwimu ni tarakimu au namba ambazo bila kupewa maana stahiki zinakuwa hazina tija yoyote hivyo ameitaka ofisi hiyo kuifanya lugha ya takwimu kuwa rafiki ili iweze kueleweka na kutumika kama ilivyokusudiwa.

“Natambua kuwa NBS imekuwa ikitoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya umuhimu wa takwimu pamoja na kuhimiza matumizi yake, hata hivyo, pamoja na jitihada zote hali halisi inaonesha kuwa bado wengi wetu hatujatoa umuhimu unaostahiki kuhusu suala la takwimu na matumizi yake kwenye kufanya maamuzi na pia kutathmini utekelezaji wa programu mbalimbali za maendeleo” ameongeza Bi. Dorothy.

[caption id="attachment_33275" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dorothy Mwanyika(kulia) akipokea nyaraka ya mkabata wa huduma kwa wateja kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa NBS, Dkt. Albina Chuwa wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), kilichofanyika leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33276" align="aligncenter" width="927"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dorothy Mwanyika akimkabidhi Kompyuta mpakato Meneja Takwimu Msaidizi wa Mkoa wa Tanga, Bi. Devotha Mdete mara baada ya kufungua Kikao cha Kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), kilichofanyika leo Jijini Dodoma. NBS imetoa vitendea kazi kwa mikoa kumi vikiwemo Kompyuta mpakato.[/caption] [caption id="attachment_33277" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dorothy Mwanyika (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza hilo leo Jijini Dodoma.[/caption]   [caption id="attachment_33278" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dorothy Mwanyika akimkabidhi cheti cha pongezi mfanyakazi hodari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Rahim Mussa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kikao cha Kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), kilichofanyika leo Jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa NBS, Dkt. Albina Chuwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya(TUGHE) tawi la NBS, Bw. Shagihilu Shagihilu.[/caption] [caption id="attachment_33279" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dorothy Mwanyika (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma.)[/caption]

Aidha, Bi. Dorothy amewataka maafisa utumishi wa ofisi hiyo kutimiza wajibu wao na kufanya kazi kwa weledi kwasababu kufanya hivyo kutarahisisha utekelezaji wa majukumu na kufikia malengo ya taasisi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu NBS Dkt. Albina Chuwa amebainisha baadhi ya mafanikio yaliyopatikana na kusema kuwa tasnia ya takwimu nchini imepiga hatua ambapo mradi wa kuboresha na kuimarisha takwimu nchini (TSMP) umesaidia kuondoa baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zikiikabili tasnia nzima ya takwimu nchini.

“Kupitia mpango huu NBS imeweza kuboresha tafiti mbalimbali za kijamii na kiuchumi na kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa kwa kutumia teknolojia za kisasa na hatimae kupunguza gharama za kufanya tafiti za kitaifa” ameeleza Dkt. Chuwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi