Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

SERIKALI: Dhamira Yetu Ni Kuona Wananchi Zaidi Wanajiendeleza Kwa Kutumia Mitandao
Jul 25, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_7436" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akiongea katika mkutano Njia Mpya za Mawasiliano Mtandaoni kati ya wadau wa Habari kati ya Tanzania na China leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Bushiri Matenda

Serikali imesema itaendelea na jitihada zake za kujenga miundombinu na kuweka mazingira wezeshi ili watanzania wengi zaidi waweze kutumia mitandao kujifunza na kushiriki katika mijadala itakayowasaidia kuwaongezea ujuzi na maarifa ili kuinua kiwango chao cha maisha.

Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na kufanya uwekezaji mkubwa katika kujenga Mkonga wa Taifa wa Mawasiliano, Serikali pia imekuwa ikichukua hatua mbali mbali kuhakikisha kuwa mitandao iko salama.

[caption id="attachment_7438" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano kuhusu Njia Mpya za Mawasiliano Mtandaoni ambapo aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika masuala Mawasiliano[/caption] [caption id="attachment_7441" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.[/caption]

“Serikali yetu imekuwa ikiendelea na hatua za kutekeleza mpango wake wa kuimarisha upatikanaji wa intaneti na usafirishaji wa data ikiwemo kuanzisha vituo vya data (data centres)”alisema Waziri huku akieleza kuwa kituo cha data cha Dar es salaam tayari kimeanza kufanyakazi.

Akifungua mkutano wa siku moja  unaohusu mitandao unaoshirikisha wajumbe kutoka Tanzania na China, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere  leo, Profesa Mbarawa amesema maendeleo ya tekinolojia ya habari na mawasiliano yamebadilisha kabisa sura na mwenendo wa vyombo vya habari hasa katika eneo la utangazaji ambapo sasa programu mbalimbali za televisheni zinapatikana kirahisi katika mitandao.

“Maendeleo makubwa katika Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano; na kuja kwa simu za mikononi kumesababisha  kuzaliwa kwa ‘taifa la mtandaoni’ ambapo wananchi wengi zaidi wanaotumia simu za mikononi wanaweza kupata habari kirahisi kutoka vyombo vya habari iwe redio, mitandao ya kijamii, majukwa ya Habari na hata televisheni” Alibainisha Waziri.

[caption id="attachment_7442" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akiteta akiwaeleza jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete (katikati) na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani.[/caption] [caption id="attachment_7443" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Waziri Mwenye Dhamana ya masuala ya mitandao kitaifa kutoka China Ren Xianliang akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano kuhusu Njia Mpya za Mawasiliano Mtandaoni ambapo aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika masuala Mawasiliano.[/caption]

Aliongeza kuwa “Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano, kama sekta inayokuwa kwa kasi sana, ina nafasi muhimu katika kuongeza upashanaji habari na katika kuongeza majukwaa ya habari” alieleza Waziri na kuongeza kuwa hiyo imesaidia upatikanaji wa habari kwa wananchi wengi zaidi.

Waziri Mbarawa alibainisha jitihada zaidi zinafanywa na Serikali kuangalia namna tekinolojia hiyo inavyoweza kutoa fursa zaidi kwa vyombo vya habari kujiimarisha na pia namna matumizi ya intaneti yanavyoweza kutumiwa kusambaza na kubadilishana habari kupitia mitandaoni.

Katika hotuba hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa wizara hiyo Steven Ngonyani, Profesa Mbarawa alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kukamilisha mradi wake wa Mkonga wa Taifa ambapo ikifikia awamu ya tano ya mradi huo itakuwa kichocheo kwa vyombo vya habari kutumia Tekinolojia ya Habari na Mawasilinao katika kutoa huduma kwa watu wengi zaidi hususan wale wanaotumia simu za mikononi.

[caption id="attachment_7444" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano kuhusu Njia Mpya za Mawasiliano Mtandaoni ambapo alisema kwa sasa serikali ipo katika hatua za kutengeneza mpango wa taifa wa Usalama wa mtandao.[/caption] [caption id="attachment_7405" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na masuala ya Mitandao China. Kutoka kulia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Rodney Thadeus (katikati).[/caption]

Alieleza kuwa Tanzania ambayo ina watu wanaotumia simu za mikononi zaidi ya milioni 39 huku wananchi wake milioni 20 wakitumia intaneti wengi wao wakiwa vijana imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa mitandao inakuwa salama.

“Hapana shaka yeyote uhalifu wa kimtandao ndio tishio kubwa kwetu na ulimwenguni kote katika matumizi ya mitandao hiyo ikiwa ni pamoja na dhamira mbaya kama udang’anyifu,wizi, kuingilia na kuharibu mifumo ya utendaji wa makampuni, udukuaji wa taarifa za kibiashara nk”

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Steven Ngonyani ametoa wito kwa wananchi kutotumia vibaya mitandao ya kijamii badala yake waitumie kujiletea maendeleo.

Alisema Kituo cha Data kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam ambacho kilichofunguliwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli hivi karibuni ni kituo muhimu katika kudhibiti mawasiliano yetu kama nchi.

[caption id="attachment_7446" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Njia Mpya za Mawasiliano Mtandaoni. (Picha na Maelezo)[/caption]

Aliongeza mchakato unaoendelea kuanzisha vituo vingine viwili kimoja Zanzibar na kimoja Makauu wa Makuu ya nchi Dodoma.

Nae, Makamu Waziri wa Habari na Masuala ya Mitandao wa Jamhuri ya Watu wa China Mr. Ren  Xianling amewaomba Watanzania na Watu wa China kutumia mitandao ya kijamii kama kichocheo cha mahusiano yenye manufaa kwa pande zote mbili.

“Ni jambo lililozoeleka kufikiria kwa jinsi gani vyombo vya habari vikiwemo  mitandao ya kijamii vinaweza kutumiwa kusaidia nchi zote mbili kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kiviwanda, alisemaNaibu Waziri huyo.

Alitoa wito kwa  wananchi wa Tanzania na China kutumia mitandao ya kijamii kutengeneza mijadala chanya ili kujenga maoni kwa umma na kushughulikia ajenda katika vyombo vya habari.

Akizungumza katika mkutano huo ambao umefadhiliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Intaneti ya China, balozi wa nchi hiyo nchini Dr. LU Yuoqing amesema  vyombo vya habari ni muhimu katika kukuza na kuimarisha uhusiano kati ya China na Tanzania na kwamba mkutano huo ni kielelezo cha ukaribu kati ya vyombo vya habari vya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ambao mada mbalimbali ziliwasilishwa na wawezeshaji kutoka China na Tanzania ulifungwa rasmi na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi