Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Lin Bin Atembelea JKCI Kuona Huduma za Matibabu ya Moyo Wanazozitoa
Jul 26, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45835" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakimsikiliza mtoto anayetibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara iliyofanywa na Naibu waziri huyo ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.[/caption] [caption id="attachment_45836" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimwelezea Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin namna ambavyo chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa watoto wenye magonjwa ya moyo kitakavyorahisisha huduma za matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri huyo alitembelea JKCI leo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.[/caption] [caption id="attachment_45837" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara fupi ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinayotolewa na Taasisi hiyo. Naibu Waziri huyo alitembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa China na kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na Hospitali kuu ya jimbo la Shandong.[/caption] [caption id="attachment_45838" align="aligncenter" width="750"] Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian Mlawi akiwaelezea Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin jinsi wauguzi wa chumba hicho wanavyowahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo.[/caption] [caption id="attachment_45839" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin akimpa pole mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.[/caption] [caption id="attachment_45840" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la nchini China Li Leping wakisaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Moja ya makubaliano hayo ni wataalamu wa afya kutoka JKCI kwenda katika hospitali hiyo kujifunza matibabu ya moyo kwa kutumia vifaa vya kisasa.[/caption] [caption id="attachment_45841" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la nchini China Li Leping wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.[/caption] [caption id="attachment_45843" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi zawadi ya ngao Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini.[/caption] [caption id="attachment_45844" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), hospitali ya jimbo kuu la Shandong na Ubalozi wa China nchini wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.(Picha na Genofeva Matemu – JKCI)[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi