Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Aishauri CBE Kutoa Vyeti kwa Wafanyabiashara.
Oct 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_20518" align="aligncenter" width="1023"]  Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wafanyakazi wa CBE alipotembelea chuoni hapo.[/caption]

Na.Mwandishi Wetu.

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya ameushauri Uongozi wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuwa na utaratibu wa kuwatambua wafanyabiashara waliofanikiwa kwa kutoa ajira nyingi kwa watanzania kwa kuwapa vyeti.

Naibu Waziri Manyanya aliyasema hayo wakati alipotembela chuo cha CBE na kuwapongeza kwa maboresho mbalimbali ambayo chuo wanayafanya ili kuboresha kiwango cha elimu chuoni hapo.

[caption id="attachment_20522" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Mhandisi Stella Manyanya wa kwanza (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa darasa la ujaliamali alipotembelea chuo cha CBE. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof.Mjema na katikati ni Mwalimu wa darasa hilo.[/caption]   Waziri alisema wakati umefika kuwatambua watu wanaofanya vizuri kwa vitendo kuthamikia kwa ubunifu wao.

“Nadhani mnatakiwa kufanya utafiti ili kutambua watu waliofanikiwa ili kuwapa vyeti ikiwezekana kuwapa hata PHD ya heshima kutokana na mchango wao wa kutoa ajira kwa watu wengi.”

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mhandishi Manyanya amekipongeza Chuo cha CBE kwa kufanya mabadiliko makubwa yanayoendana na wakati.

“Kwa mabadiliko haya yaliofanyika yamenifurahisha, hata mwanafunzi akikwambia anatotoka chuo cha biashara anaeleweka, tuwafundishe wanafunzi wetu wayaishi yale yanayoonekana”.

Alisisitiza kuwa chuo hicho ni muhimu katika kuwabadilisha vijana kuwa na mtazamo wa namna wanavyofanya shughuli zao katika kuelekea katika uchumi wa Viwanda na pia kupata ujasiri katika kuanzisha biashara.

“Natamani mitaala yetu irudi katika utendaji wa vitendo, tuwafanye vijana wetu waungane na watu wa mataifa mengine katika kuanzisha biashara”

Aliwataka pia wahadhiri wa chuo hicho kuwatafutia wanafunzi namna ya kukutana na wajasiriamali wadogowadogo, ili waweze kupata ujuzi na pia kuwasaidia wajasiriamali hao kupata njia bora za biashara.

“Chuo kiwaandae vijana katika kuwajengea mazingira ya kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa peke yake,” alisema Naibu waziri Mhandisi Manyanya.

Akimkarisha Naibu Waziri, Mkuu wa Chuo hicho Prof.Mjema alisema kuwa mbali na mafanikio waliyofikia, bado wana changamoto ya kuwa na uhaba wa fedha za kujiendesha, na uchakavu wa majengo chuoni hapo.

“Uchache wa wafanyakazi, uvamizi wa baadhi ya maeneo ya chuo,pamoja na upungufu wa wanafunzi wanadahiliwa chuoni ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili chuo kwa sasa.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi