[caption id="attachment_49436" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akicheza ngoma ya asili na vijana wa jamii ya Kiiraiqw waliyoshiriki shindano la Mr.Mayo na Miss Imbori ambao wanahistoria katika jamii hiyo katika masuala ya mila na desturi leo katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere Wilayani Mbulu wakati wa sherehe za kufunga Tamasha la nne la Utamaduni na Michezo la jamii hiyo lililoandaliwa na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu.[/caption]
Na Anitha Jonas – WHUSM,Mbulu Manyara.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa wadau mbalimbali katika jamii kujitokeza kuandaa matamasha ya kufundisha vijana katika kuhusu maadili, mila na desturi nzuri.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Wilayani Mbulu alipokuwa akifunga Tamasha la Nne la Utamaduni na Michezo la Jamii ya Wairaiq lilolenga kutoa piga vita mila potofu na kutoa kuwafundisha vijana wa jamii hiyo maadili,mila na desturi za jamii hiyo ili waweze kuzitunza na kuzienzi .
Akiendelea kuzungumza katika tamasha hilo Naibu Waziri huyo aliendelea kutoa wito kwa vijana wa jamii hiyo kuhakikisha wanazingatia malengo ya tamasha hilo ikiwepo kuzingatia suala la uwajibikaji na kuchapa kazi na pia kuacha masuala ya ulevi.
“Kila jamii katika taifa letu ikijipanga kufanya tamasha kama hili la utamaduni kwa vijana hakika tutajenga taifa bora lenye nidhamu,uwajibikaji na wachapakazi na hii itasadia sana kupunguza wahalifu katika jamii yetu,”amesema Mhe.Shonza.
Pamoja na hayo Naibu Waziri huyo mwenye dhamamana ya utamaduni na michezo alitoa pongezi kwa uongozi wa Kanisa Katoliki Wilaya ya Mbulu kwa kuandaa tamasha hilo lenye tija kwa vijana ambao ndiyo taifa la kesho pamoja na Redio Habari Njema inayosimamiwa na kanisa hilo kwa kuelimisha umma kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo mila na desturi.
[caption id="attachment_49439" align="aligncenter" width="1000"]Kwa upande wa Mhasham Askofu Mkuu Jimbo la Kanisa Katoliki Mbulu Anthony Lagweni Gaspar ambaye ndiyo kiongozi mkuu aliyoratibu tamasha hilo alitoa ombi kwa serikali kwa kuomba kuanzishwe kituo cha kutunzia kumbukumbu za kimila na kuhifadhi zana mbalimbali za jadi ikiwemo vifaa vya muziki wa asili kama marimba.
“Kuwepo kwa kituo kinachoelezea historia,utamaduni,mila na desturi za watu wa jamii ya kiiraiq katika wilaya hii ya mbulu kutasaidia kuongeza mapato kupitia watalii na kutangaza asili jamii hii pamoja na umahiri watu wake katika mchezo wa riadha,’’alisema Mhasham Askofu Gaspar.
[caption id="attachment_49441" align="aligncenter" width="1000"]Halikadhalika Askofu huyo aliendelea kusema kuwa kupitia tamasha hili tunapenda kukemea fikra za vijana za kuto wajibika na badala yake kusubiri kurithishwa mali za wazazi tunataka vijana waache uvivu na zaidi wajitume kutafuta mali zao wenyewe badala ya kutegemea mali za wazazi.
Naye Mbunge Mbulu Vijijini Bw.Flatei Massay alishukuru uongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa juhudi kubwa wanayofanya ya kusimamia masuala ya Michezo na Utamaduni kwa sasa.