Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Nishati Awapa Saa 6 TANESCO, Kurejesha Hali ya Kawaida Mitambo Iliyopata Hitilafu Ubungo I
Sep 29, 2023
Naibu Waziri Nishati Awapa Saa 6 TANESCO,  Kurejesha Hali ya Kawaida Mitambo Iliyopata Hitilafu Ubungo I
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga (kushoto), akiwa katika chumba cka kuendeshea mitambo cha Ubungo II akionyeshwa namna umeme unavyopokelewa, kupoozwa na kusambazwa katika kituo hicho wakati wa ziara yake Septemba 29, 2023 jijini Dar es salaam.
Na Zuena Msuya, DSM

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amelipa saa sita Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuirejesha katika hali ya kawaida ya uzalishaji mitambo iliyopata hitilafu katika kituo cha Ubungo I.

Kapinga amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua hali ya uzalishaji wa umeme katika Vituo vya Kupoza na Kusambaza Umeme vya Ubungo I na Ubungo II ili kuona hali ya uzalishaji katika vituo hivyo, Septemba 29, 2023 jijini Dar es salaam.

Aliwaeleza kuwa, kutokana na changamoto ya upatikanaji wa umeme nchini, ni vyema  TANESCO wakaweka mpango wa kufanya marekebisho ya muda mfupi, wakati na muda mrefu katika mitambo, na marekebisho hayo yafanyike kwa wakati na muda sahihi ili kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata umeme wa uhakika wakati wote.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshatoa maelekezo kuwa matengenezo yafanyike ndani ya miezi sita yakamilike, sisi kama Wizara tunasimamia na kuhakikisha kuwa kila mashine ambayo inatakiwa kufanyiwa marekebisho inafanyiwa marekebisho hayo na yanamilika kwa wakati”, alisema Kapinga.

Kapinga alifafanua kuwa mashine zenye hitilafu husababisha upungufu katika usambazaji wa umeme na hivyo watumiaji kuilaumu Serikali juu ya hali hiyo.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri huyo amekagua kituo cha Ubungo II chenye mitambo mitatu ambapo kati ya hiyo, huko kwenye matengenezo na Katika kituo cha ubungo I chenye mashine 12, ambapo sita zinafanya kazi na nyingine ziko kwenye matengenezo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi