Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Nishati Akerwa na Mkandarasi Mbabaishaji
Feb 25, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_40800" align="aligncenter" width="1000"] Mkazi wa kijiji cha Mkwanyule, Kata ya Masoko, wilayani Kilwa, Rehema Sudi (kulia), akitoa maoni yake kuhusu masuala ya umeme, kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba), wakati wa ziara yake eneo hilo jana, Februari 24, mwaka huu.[/caption]

Na Veronica Simba – Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amekemea vikali utendaji kazi mbovu wa Mkandarasi State Grid, anayetekeleza mradi wa umeme vijijini Mkoa wa Lindi kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kutokamilisha wigo wake kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nangambi Naipuli, Kata ya Mingumbi, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi, jana Februari 24, mwaka huu, Naibu Waziri alisema Serikali imemvumilia kwa muda mrefu Mkandarasi huyo, ambaye pia anatekeleza mradi huo katika Mkoa wa Morogoro.

Kufuatia utendaji huo duni wa mkandarasi husika, Naibu Waziri alikataa kuwasha umeme katika kijiji hicho, kama ilivyokuwa imepangwa, na kuelekeza kuwa atafanya zoezi hilo pale ambapo idadi ya wananchi waliounganishiwa umeme itakapokuwa ya kuridhisha, tofauti na idadi ndogo ya waliounganishiwa sasa ambayo ni watano tu.

[caption id="attachment_40801" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba – katikati), akiwa katika usafiri wa Boti ndogo pamoja na Ujumbe wake, kuelekea Kilwa kisiwani, mkoani Lindi, jana Februari 24, mwaka huu akiwa katika ziara ya kazi.[/caption]

“Huu ni utapeli mtupu, mimi sitafanya kazi hii. Siwashi umeme na naenda kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika kwamba mkandarasi anababaisha.”

Akifafanua, Naibu Waziri alieleza kuwa Mkandarasi huyo amekuwa mwenye kiburi na asiyejirekebisha na kwamba taarifa za utendaji wake mbovu tayari zinafahamika hadi wizarani hivyo hakuna haja ya kuendelea kumvumilia, bali ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.

Kufuatia hali hiyo, Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilwa, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai, alimtaka Mkandarasi husika kuripoti ofisini kwake siku ya Jumatano, Februari 27 mwaka huu, akiwa na Hadidu za Rejea ili pamoja na mambo mengine, akaeleze amejipanga vipi kukamilisha kazi husika ndani ya muda wa makubaliano.

Awali, Naibu Waziri Mgalu alitembelea na kukagua Kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia cha Somanga kilichopo wilayani Kilwa, ambapo alieleza kwamba Serikali imedhamiria kupeleka umeme wa uhakika na wa kutosha katika mikoa yote ya Kusini.

[caption id="attachment_40802" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba cha kijani), akiwasili Kilwa kisiwani, mkoani Lindi, kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, jana Februari 24, mwaka huu.[/caption] [caption id="attachment_40803" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (mwenye kinasa sauti), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nangambi Naipuli, Kata ya Mingumbi, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi, jana Februari 24, mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi.[/caption]

Aidha, Naibu Waziri alitembelea pia vijiji vya Kisangi na Mkwanyule pamoja na Kilwa Kisiwani ambapo alizungumza na wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya umeme pamoja na kupokea kero zao.

Akiwa Kilwa Kisiwani, alimsisitiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Jua mahala hapo, ambaye ni Kampuni ya Green Leaf, kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo kwa wakati, kabla ya Juni 30 mwaka huu, ambapo Mkataba wake utakwisha.

Naibu Waziri yuko katika ziara ya kazi ya siku Nne mkoani Lindi, ambayo aliianza jana, Februari 24, mwaka huu. Katika ziara hiyo, amefuatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi