Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Mwinjuma, Hakimiliki Ghana Wabadilishana Uzoefu Masuala ya Hakimiliki
Mar 11, 2024
Naibu Waziri Mwinjuma, Hakimiliki Ghana Wabadilishana Uzoefu Masuala ya Hakimiliki
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma akizungumza na Maafisa wa Ofisi ya Hakimiliki ya nchini Ghana ikiongozwa na Ndg. William Bonsu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na baadhi ya wataalamu wa Hakimiliki wa nchi hiyo.
Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amekutana na kufanya mazungumzo na Ofisi ya Hakimiliki ya nchini Ghana ikiongozwa na  Ndg. William Bonsu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na baadhi ya wataalamu wa Hakimiliki wa nchi hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Machi 11, 2024 katika ofisi hizo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Hakimiliki ikiwemo ukusanyaji na ugawaji wa  mirabaha pamoja na sheria mbalimbali za Hakimiliki kwa kazi za ubunifu.

Ndg. William Bonsu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria  ya nchini Ghana  (kushoto)  akijadili jambo na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma 

Wamefanikiwa kujifunza namna nchi hiyo inavyokusanya mirabaha kwa kutumia Kampuni za Kukusanya na Kugawa Mirabaha (COLLECTIVE MANAGEMENT ORGANISATION -CMO'S) na kuzisimamia ambapo pia Tanzania inafanya jambo kama hilo kwa Wasanii na Wabunifu kupitia taasisi ya TAMRISO inayokusanya mirabaha ya wanamuziki.

Kikao hicho kimefanyika kando ya Mashindano ya Michezo ya Afrika (All African Games) yanayoendelea nchini humo ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 zinazoshiriki michezo hiyo

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi