Naibu Waziri, Mhe. Khamis Hamza Ateta na Mjumbe kutoka Serikali ya Uingereza
Nov 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mjumbe kutoka Serikali ya Uingereza, Bi. Janet Rogan akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis na ujumbe wake katika kikao cha ushirikiano kilichofanyika katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri leo tarehe 16 Novemba 2022.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Bi. Patricia Scotland katika banda la Tanzania kwenye Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri. Bi. Scotland, ameipongeza Tanzania kwa jitihada za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.