[caption id="attachment_50490" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisisitiza jambo alipozungumza na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Songwe.Anayemuangalia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemus Mwangela.[/caption]
Na Munir Shemweta, WANMM ILEJE
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutenga bajeti kwa ajili ya Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji sambamba na kufuatilia tozo zinazotozwa na Mabaraza hayo ili yafanye kazi kwa ufanisi.
Dkt Mabula alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wilayani Ileje na Mbozi wakati akizungumza na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na ujenzi wa miradi inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Songwe.
Naibu Waziri Mabula alisema, Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wamekuwa hawatengi bajeti kwa ajili ya Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji jambo linalosababisha Wajumbe wake kujifanyia mambo wanavyotaka ikiwemo kuweka viwango tofauti vya tozo za kwenda uwandani.
[caption id="attachment_50489" align="aligncenter" width="750"]Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji yanapaswa kusimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri kwa kuyapatia kwa kuyatengea bajeti za kuendesha ofisi kama vile Shajala sambamba na kujua yanayofanyika ikiwemo tozo zake ili kuepuka uonevu unaoweza kujitokeza kwa wananchi wanaoshitakiana.
‘’Katika Mabarza ya Ardhi ya Kata na Vijiji watu wanalipa tozo kulingana na sura kama mtu kavaa tai basi anapigwa shilingi elfu hamsini jambo linalowaumiza wananchi’’ alisema Mabula
Alizitaka ofisi za Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuyasimamia Mabaraza hayo na kutoa semina kwa wajumbe wake na kuyapangia viwango vya tozo na kusisitiza kuwa hayo yasipofanyika kuna hatari wajumbe wake kufanya maamuzi kwa matakwa ya wenye uwezo.
Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kubadilika katika kuyasimamia mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji na kubainisha kuwa Mabaraza hayo yakifanya vizuri yatapunguza mlundikano wa kesi za ardhi zinazokwenda Mabaraza ya ardhi ya nyumba ya Wilaya.
[caption id="attachment_50491" align="aligncenter" width="900"]Akikagua maendeleo ya ujenzi huo, Dkt Mabula mbali na kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo alisema mradi wa ujenzi wa ofisi na nyumba ya Meneja wa TFS utasaidia ufuatiliaji wa msitu huo kwa kuwa Meneja wake atakuwa akiishi karibu na msitu huo. Aidha, ameuelezea mradi huo kuwa umesaidia pia kutengeneza ajira ya muda kwa wakazi wa eneo hilo na kuwawezesha kupata kipato cha mahitaji madogomadogo.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Mbeya Pauline Kamaghe alisema mradi huo unaojengwa na Shirika lake unatarajiwa kugharimu kiasi cha milioni 426.8 na kukamilika mwezi April mwaka huu wa 2020 na kubainisha kuwa kwa sasa mradi umefikia asilimia 38 ya ujenzi.
[caption id="attachment_50492" align="aligncenter" width="750"]