Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF.
Sep 18, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_14294" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akiongea na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Viongozi toka Wizarani pamoja na Wadau wa soka wakati alipotembelea ofisi za Shirikisho hilo kujionea namna wanavyotekeleza majukumu yao katika kuleta maendeleo katika soka 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ufanisi wao wa kazi huku akiwataka kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Awamu ya Tano ili kuleta maendeleo katika soka.

Mhe. Wambura ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi za Shirikisho hilo ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ikiwemo changamoto za shirikisho pamoja na maendeleo ya soka nchini.

Akiongea na Viongozi mbalimbali na wadau wa soka katika ziara yake hiyo, amesema kwamba anaridhishwa na kazi wanazofanya TFF na amewapongeza kwa kupata uongozi mpya wa Shirikiho hilo na kuwasisitizia kujenga mahusiano ya karibu na wadau wa soka ikiwemo kuwajengea uwezo vijana ili kukuza vipaji vyao na hatimaye kuleta heshima kwa Taifa.

[caption id="attachment_14295" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura(aliyekaa katikati) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwemo wengine toka Wizarani wakiwaangalia vijana wa Serengeti Boys wanaochipukia wakifanya mazoezi katika Viwanja vya Karume 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.[/caption]

“TFF hongereni kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya, hakika mnajitahidi sana lakini niwaombeni muzidi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kwamba tunapata maendeleo mazuri katika soka, hivyo ni vema mkawa mnajenga mawasiliano na Viongozi wa Serikali mara kwa mara ili na sisi tupate kujua mambo yanayofanyika”, alisema Mhe. Wambura.

Sambamba na hilo, Naibu Waziri Wambura amesisitiza juu ya suala la ugawaji wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira ya kuchezea katika maeneo mbalimbali nchini huku akisema kuwa, ugawaji huo uwe wa uwiano sawa ili pasitokee eneo moja likawa linakosa vifaa hivyo kwakuwa vijana wote ni Watanzania na wana haki sawa ya kushiriki katika michezo.

[caption id="attachment_14293" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akiongea na Vijana wa Serengeti Boys wanaochipukia wakati alipotembelea Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Bw. Kidao Wilfred amesema kwamba, TFF imejitahidi kuwasaida vijana mbalimbali wakiwemo Serengeti Boys kwa kuwapatia vitendea kazi na amepokea ushauri wa Naibu Waziri wa kuendelea kujenga uhusiano wa karibu na Serikali ili kukuza soka nchini.

“TFF tumekuwa tukiwaandaa vijana mbalimbali ili kuweza kuwapata wenye vipaji vizuri na tumepanga kuwa vijana hawa waweze kupatiwa shule ambapo watakuwa wanajifunza masuala mazima ya soka na nikieleze tu Mheshimiwakwamba ushauri wako wa kujenga ushirikiano na Serikali tumeupokea na tunaufanyia kazi”, alisema Wilfred.

[caption id="attachment_14296" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akisalimiana na Kocha Kim Paulsen wakati alipotembelea ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.[/caption]

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi