Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Katibu Nishati Akagua Miundombinu ya Gesi Songosongo
Apr 01, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Zuena Msuya, Lindi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ametembelea na kukagua miundombinu ya Mradi wa kuzalisha na kuchakata Gesi asilia wa Songosongo uliopo mkoani Lindi.

Mahimbali amesema kuwa lengo la ziara hiyo iliyofanyika Machi 31, 2022 ni kutaka kuona shughuli za uzalishaji, uchakataji na usafirishaji wa Gesi asilia kutoka katika visima vya Gesi vilivyopo katika eneo la bahari na nchi kavu katika eneo hilo.

Katika ziara hiyo, ametembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Songosongo, eneo lililofungwa mtambo mpya wa kuongeza mgandamizo wa Gesi asilia, pamoja na Kisima namba kumi kinachofanyiwa ukarabati.

Aidha, alitembelea kisima namba nne, 12, 11 pamoja na sehemu ambayo gesi inayozalishwa kutoka visimani inasafirishwa kuingia katika bomba la kusafirisha Gesi asilia kwenda Somangafungu hadi Kinyerezi, Dar es salaam kwa ajili ya kuzalisha Umeme na matumizi mengine.

Eneo lingine alilotembelea ni eneo la kupokelea gesi kutoka katika visima vya gesi inapochakatwa, sehemu ya kuongeza mgandamizo wa gesi asilia (compression) pamoja na chumba maalum cha kuendeshea mitambo ya gesi asilia (Control room).

Katika ziara hiyo ameambatana na Viongozi Waandamizi kutoka Wizarani na Kampuni Tanzu ya kusimamia Gesi (GASCO) ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Picha mbalimbali zikimuonyesha Naibu Katibu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya mradi wa gesi asilia ya Songosongo mkoani Lindi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi