Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MNH Yaokoa  Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nje ya Nchi.
Sep 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na. Paschal Dotto 

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mionzi (Radiolojia) imeokoa zaidi ya bilioni 3.96 kwa kuanzisha huduma ya kutibu wagonjwa wenye uvimbe kwa kutumia vifaa vya mionzi huduma ambayo awali haikuwepo nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Praxeda Ogweyo amesema kuwa huduma hiyo ambayo ilianza rasmi Oktoba mwaka jana mpaka sasa wagonjwa 45  wametibiwa.

“Kabla ya kuanzishwa kwa huduma hii wagonjwa wengi walikuwa wakienda nje ya nchi has India ambapo walikuwa wanalipa gharama kubwa sana, lakini kwa sasa huduma hii inapatikana hapa nchini kwa hiyo watanzania wenye matatizo ya uvimbe waje wapate huduma hii kwa gharama nafuu ya milioni 2 kwa kila awamu”, alisema Dkt Ogweyo.

Dkt, Ogweyo alisema kuwa kati ya wagonjwa 45 waliotibiwa wamegharimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi milioni 360 tofauti na kupata huduma hii nje ya nchini ambayo ingeweza kugharimu takriban shilingi bilioni 4.320.

Aidha Dkt Ogweyo aliongeza kuwa huduma hii inahusisha utaalam wa vifaa vya mionzi (Radiolojia) kama vile X-Ray, MRI, CT- scan na Ultra-sound kutibu kabisa ugonjwa au kuchukua sampuli kwa uchunguzi zaidi.

Akiainisha huduma ambazo zinatolewa mpaka sasa na kitengo hicho Dkt. Ogweyo alisema ni pamoja na kuondoa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa, uso na shingo (Haemogioma na Lymphongioma), kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya mikojo imeziba, huduma ya kuzibua mirija ya uzazi na kunyonya usaha kwenye uvimbe ulioko tumbuni.

Dkt. Ogweyo alibainisha  kuwa kabla ya huduma hii wagonjwa wenye matatizo hayo iliwalazimu kwenda kutibiwa India kwa gharama kubwa zaidi ambayoya shilingi  milioni 96 kwa mgonjwa mmoja lakini kwa hapa nchni ni shilingi milioni 8 tu.

Naye Mkuu wa Idara ya Radiolojia Dkt. Flora Lwakatale amaipongeza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuanziaha huduma hii nchini.

“Ni furaha na fahari kubwa kwa nchi yetu kwa kuweza kuanzisha huduma hii nchini naipongeza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuweka juhudi katika hili, nawakaribisha watanzania wote tupo tayari kutoa huduma ya matibabu hayo”,  Dkt. Lwakatale.

Kwa upande wao wanufaika wa huduma hii Leyla Mauld na Joan Nico wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuboresha huduma za afaya nhini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi