Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani Rungwe.
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka mmiliki wa kiwanda cha kupaki maparachichi cha Rungwe overcado Company, kuongeza bei na maslahi kwa wafanyakazi na wakulima wa zao hilo.
Akizungumza kiwandani hapo, katika mwendelezo wa ziara yake ya siku nane Mkoani Mbeya, Rasi Magufuli amesema kuwa Serikali iko tayari kuwasikiliza wawekezaji ili kuwawezesha wakulima kupata faida kubwa kutoka katika uwekezaji pia makampuni kuongeaza bei kwa wakulima ili waongeze kipato.
“Serikali itaendelea kwashika mkono wakulima na wawekezaji kwa ujumla, tutaendelea kusikiliza shida za wawekezaji kutoka katika maeneo yao ya uwekezaji, lakini wakati Serikali inashughulikia shida zao, niwaombe wawekezaji nao washughulikie shida za walipa kodi hawa kwa kutoa bei nzuri ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya wafanyakazi ili tuende sawa”, alisema Rais Magufuli.
Akizundua kiwanda hicho kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Rais Magufuli ameishukuru kampuni ya Rungwe overcado Company kwa kujenga kiwanda cha kisindika na kupaki zao la parachichi kwani itawasaidia wakulima kupata sehemu ya kupeleka mazoa yao
Aidha, Rais Magufuli aliishukuru bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kwani wameanzisha kiwanda ambacho kiwasaidia wanachi 20,000 wanaoilima zao la parachichi Wilayani Rungwe.
“Nawashukuru sana bodi ya wakurugenzi kwa kiwanda hiki, nimeona teknolojia inayotumika ni ya kisasa zaidi, lakini pia mmeweza kuwasidia wakulima hawa 20,000 ambao walikua wakihangaika na zao hili pindi wanapovuna hongereni sana.”, Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliongeza kuwa kampuni hiyo imewekeza baada ya Serikali kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo upatikanaji wa umeme, lakini pia ujenzi na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songwe ambacho kitakuwa kiungo muhimu wakati wa usafirishaji wa maparachichi.
Akiwa kwenye zaiara hiyo Rais Magufuli alitatua baadhi ya kero za wananchi wa eneo la Katumba kwa kutoa shilingi milioni tano ambazo ni mchango wake wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Tuso, huku akiwaasa wananchi wa eneo hilo kuiacha shule hiyo iendelee kuwa mikononi mwa kanisa la wasabato.
Aidha alwasihi waache ugomvi katika kutekeleza maendeleo kwani ugomvi huchelewesha maendeleo “Masuala ya ugomvi hayafai kwenye maendeleo, yanachelewesha maendeleo kwenu kwa hiyo nawaomba muache masuala haya na muendelee kuchapa kazi kuleta maendeleo.”, alisisitiza Rais Magufuli.
Akiwa Wilayani Busokelo, Rais Magufuli alisema kuwa katika halmashauri hiyo serikali imetekeleza ujenzi wa vituo vitatu vya afya kwa gharama ya Tsh. Bilioni 1.4, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Busokelo itakayogharimu Tsh.Bilioni 2, lakini kwa kutambua umuhimu wa wakulima kutoka wilaya ya busokelo alizindau kilometa 10 za barabara na kutoa maelekezo kwa Wizara ya Ujenzi kuanza mchakato wa ujenzi wa Kilometa 71 za barabara katika halmashauri ya wilaya hiyo.
“Huku ni maeneo ambayo watu ni wazalishaji, na mazao yote yanakubali, ninafahamu katika bajeti ya mwaka huu hapa tunatakiwa kuanza na kilometa 17, lakini naomba niseme kwa dhati kwamba tutaitengeneza barabara yote kilometa 71 kwa kiwango cha lami, hatuwezi kushindwa kilometa hizo ni chache, Serikali hii siyo ya kushindwa kujenga barabara.” Alisema Rais Magufuli.
Katika kero ya Maji Wilayani Busokelo, Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa alisema kuwa mradi ambao ulianzhishwa mwaka 1968, Serikali iko tayari kuutekeleza na kwamba fedha zimetengwa Tsh.Bilioni 1.5, kilichobaki ikiwa ni halmashauri ya wilaya hiyo kutekeleza mradi huo wa siku nyingi.
MWISHO.