Mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Mabunge ya Afrika
Nov 01, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Washiriki wa mkutano wa sita wa Wanasheria wa Mabunge ya Afrika kutoka nchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo nje ya Jiji la Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa sita wa Wanasheria wa Mabunge ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo nje ya Jiji la Zanzibar ( kulia) ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemedi Suleiman Abdulla, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt.Mwinyi Talib Haji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akipokea kitabu kutoka kwa Bw. Mussa Kombo Bakari, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Mabunge ya Afrika baada ya kufungua mkutano wa sita wa Wanasheria wa Mabunge ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemedi Suleiman Abdulla akipokea kitabu kutoka kwa Bw. Mussa Kombo Bakari, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Mabunge ya Afrika baada ya ufunguzi mkutano wa sita wa Wanasheria wa Mabunge ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akifuatana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman Abdulla baada ya ufunguzi wa mkutano wa sita wa Wanasheria wa Mabunge ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr (kulia) ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa.