[caption id="attachment_36389" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza katika eneo la utekelzaji wa mradi wa maji chalinze wakati wa ziara yake yakukagua hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo ambapo amemtaka mkandarasi kukamilisha mradi huo ifikapo Desemba 31, 2018. Na; mwandishi wetu[/caption]
Mkandarasi wa mradi wa maji Chalinze ametakiwa kukamilisha mradi huo kufikia mwezi Desemba mwaka huu ili wananchio waweze kupata huduma iliyokusudiwa ya maji safi na salama kama Serikali ilivyokusudia.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika eneo la mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa mkandarasi huyo tayari ameshaongezewa muda mara 3 lakini bado ameshindwa kukamilisha mradi huo hivyo anatakiwa kukamilisha mradi huo katika katika muda huo.
" Mkandarasi ametueleza changamoto mbalimbali zinazomkabili ambazo kimsingi hazikubaliki na tunachotaka ni mradi huu ukamilike ifikapo Desemba 31 mwaka huu"; Alisistiza Mwamunyange.
[caption id="attachment_36390" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange ( katikati) akiendelea kukagua miundo mbinu inayojengwa katika chanzo cha maji cha mradi wa maji Chalinze kilichopo mto wami.[/caption] [caption id="attachment_36391" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Msimamizi wa mradi wa maji Chalinze Mhandisi Modester Mushi akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange wakati alipotembelea mradi huo kujionea hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake.[/caption] Akifafanua amesema kuwa hatua mbalimbali zimechukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika ili uweze kuwanufaisha wananchi. Utekelezaji wa mradi huo utasaidia kuinua uchumi wa wananchi na kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda katika mkoa wa Pwani na maeneo ya jirani ya mkoa wa Tanga.(Picha zote na DAWASA)