Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Miradi 106 ya Maji Yafanikisha Azma ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani
Mar 20, 2025
Miradi 106 ya Maji Yafanikisha Azma ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bi. Lilian Mbassy akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Benki hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.
Na Frank Mvungi, Dodoma

Miradi 106 ya maji iliyofadhiliwa na Benki ya Maendeleo TIB imeleta matokea chanya kwa Mamlaka za Maji 10 na Jumuiya za Watumiaji Maji Vijijini 96.

Akieleza mafanikio ya Sekta hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo amesema kiasi cha shilingi bilioni 22.4 zimewekezwa katika mikoa 12 .

"Wananchi 870,648 wamenufaika na miradi ya majisafi na salama", alisema Bi  Mbassy

Ameitaja mikoa 12 iliyonufaika na uwekezaji huo kuwa ni Dodoma, Singida, Shinyanga, Tanga, Mtwara, Iringa, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Dar es Salaam, Kagera na Mara.

Akifafanua, amesema uwekezaji huo umetumia kilomita 425 za mtandao wa usambazaji wa maji katika mikoa 12.

Matokeo ya uwekezaji huo kupitia Mamlaka za maji amesema ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa majisafi na salama na kupunguza milipuko ya magonjwa na kumtua ndoo mama kichwani.

Mwelekeo wa Benki Maendeleo TIB katika Sekta ya maji ni kuendelea na uwekezaji kupitia Mamlaka za Maji na kufanya kazi na taasisi za Serikali na Jumuiya ya Maendeleo kama Mfuko wa Maji wa Taifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi