Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Milioni 780 Kujenga Kliniki ya Huduma za Methadone Mkoa wa Tanga
Jun 25, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53570" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisema jambo wakati wa uzinduzi wa kliniki ya huduma za methadone Mkoa wa Tanga[/caption]

Na WAMJW - Tanga

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea kuboresha huduma za afya nchini ambapo shilingi milioni 780 zimetolewa kwa ajili ya kujenga kliniki ya huduma za methadone kwa waathirika wa madawa ya kulevya mkoani Tanga.

[caption id="attachment_53571" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela akisema jambo wakati wa uzinduzi wa kliniki ya huduma za methadone kwa Mkoa wa Tanga.[/caption]

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kituo cha muda cha kutoa tiba ya methadone kwa warahibu wa madawa ya kulevya kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga - Bombo.

“Kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo Mfuko wa Dunia (Global Fund) na Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya tumepata zaidi ya milioni 780 na tumezileta kwa ajili ya kujenga jengo la kutolea huduma ya methadone” amesema Waziri Ummy.

[caption id="attachment_53572" align="aligncenter" width="750"] Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Jamesi Kaji akisema jambo wakati wa uzinduzi wa kliniki ya huduma za methadone mkoani Tanga.[/caption]

Hata hivyo waziri Ummy Mwalimu hakusita kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Tanga kwa ubunifu walioufanya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo PEPFAR na Amref -Tanzania, kwa kujenga kituo cha muda kwa ajili ya kutoa tiba kwa warahibu wa madawa ya kulevya ambacho kimegharibu shilingi milioni 20 za Kitanzania.

“Tumeona tunaweza kufanya huduma hizi kwa gharama nafuu, ninafurahi kuona kwamba zimetumika takribani shilingi milioni 20 kwa ajili ya kutengeneza kituo cha muda kwa huduma za kliniki katika Mkoa wa Tanga” amesema Waziri Ummy.

[caption id="attachment_53573" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya wakipongeza kwa furaha wakati Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela akimpatia dawa ya methadone kwa mnufaika wa huduma hiyo iliyozinduliwa mkoani humo.[/caption]

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa ilikuwepo haja ya kuwa na kliniki ya methadone kwa Mkoa wa Tanga kutokana na kuwa na waathirika wengi wanaotumia madawa ya kulevya huku mkoa huo ukishika nafasi ya pili ya kuwa nawarahibu wengi wa madawa ya kulevya.

“Mkoa wa Tanga unashika nafasi ya pili ya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa madawa ya kulevya, takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha Mkoa wa Tanga una watumiaji taribani 5190 wa madawa ya kulevya” amefafanua Waziri Ummy Mwalimu

Waziri Ummy amesema kuwa hadi sasa kuna kliniki 8 ambazo zinatoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa Mkoa wa Dar Es Salaam kliniki hizo zimeanzia katika hospitali ngazi ya mikoa na kushuka chini kwenye hospitali za ngazi ya halmashauri na kutaja maeneo yatakayofuata kuwa na huduma hizo ni pamoja na Bagamoyo, Kigamboni, Mbagala, Tegeta pamoja na Magereza Segerea.

[caption id="attachment_53574" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akifurahi mara baada ya kuzindua kliniki ya huduma za tiba ya methadone katika Mkoa wa Tanga, kushoto ni mnufaika wa huduma hiyo akipata tiba.[/caption]

Amesema kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya, Tanzania ina waathirika 8,071 wanaopatiwa huduma ya dawa za methadone kwa ajili ya kupunguza madhara ya dawa za kulevya ambapo kati yao wagonjwa 480 ni wanawake na 7,591 ni wanaume.

Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Bw. James Kaji amesema kuwa wiki hii Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya kupinga madawa ya kulevya ambayo kwa mwaka huu kauli mbinu ni "tujenge uelewa sahihi kwa tatizo la dawa za kulevya ili kuimarisha mapambano dhidi ya tatizo hilo".

“Uzinduzi wa kituo hiki ni muendelezo wa vituo vingine 8 vinavyotoa huduma nchini ambapo kwa Dar es Salaam vipo vitatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Temeke; Mbeya – Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini; Mwanza – Hospitlai ya Rufaa ya Sekou Toure; Bagamoyo na Dodoma – Itega” amefafanua Kamishna Jenerali James Kaji

[caption id="attachment_53569" align="aligncenter" width="750"] Ujenzi wa jengo la kliniki ya huduma za tiba ya madawa ya kulevya katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga ukiendelea ambapo ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 780 za kitanzania.[/caption]

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martin Shigela amesema kuwa Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya shughuli za usafirishaji wa madawa ya kulevya na kufanya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji ambao huingia kwenye urahibu wa madawa hayo.

Aidha Mhe. Shigela ameiasa jamii kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya huku akiwaomba kutoa taarifa kwa mamlaka kwa wale wanaojihusisha na usafirishaji na biashara ya madawa ya kulevya.

“Kwa wale ambao wameathirika na madawa ya kulevya katika jamii zetu tuwaone ni kama sehemu ya ndugu zetu, tusiwanyanyapae, tuwaelekeze na tuwalete kwenye matibabu na tunaamini watarudi kwenye hali ya kawaida” amesisitiza Mhe. Shigela

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi