Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mpwapwa Watakiwa Kutoa Maelezo kwa Kununua Dawa Nje ya MSD
Dec 09, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na Catherine Sungura.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa  Dkt. Said Mawji na Meneja wa Bohari Kuu ya Dawa Kanda ya Kati (MSD) Helman Mng'ong'o wametakiwa kuandika ripoti na kuifikisha kwa Naibu Waziri wa Afya  siku ya jumatano wakieleza kwanini pesa nyingi za dawa zinatumika kununua dawa kwa mshiriti badala ya bohari ya dawa.

Agizo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya, DKt. faustine Ndugulile kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Mpwapwa mara baada ya kupokea ripoti ya afya ya wilaya hiyo

Katika taarifa ya Mganga Mkuu wa Wilaya inaonyesha kati ya shilingi milioni 57 walizopewa za kununua dawa kwenye vituo vya afya ni shilingi laki 7 tu ndo zimetumika kununulia dawa MSD.

"Kwanini fedha za vituo na zahanati zinaenda kununua dawa nje?hili ni tatizo kubwa hapa, kwahiyo MSD ni wabia wa kushiriki kununua dawa nje.

Alishangaa kusikia meneja wa MSD akisema kwa kipindi cha miezi ya Julai hadi Septemba ni aina nne tu za dawa ndizo hazikuwepo Bohari Kuu lakini inaonesha dawa nyingi zimenunuliwa nje ya MSD.

"Fedha za dawa ni za kuziogopa sana, naenda kulifuatilia hili, nahitaji ripoti kwani kwa ripoti ya Julai hadi Septemba Mpwapwa hali ya upatikanaji wa dawa mlikua ni asilimia 79.

Hata hivyo dkt. Ndugulile alisema wizara inatarajia kuwa na dawa muhimu zaidi ya 135 ziwepo kwenye bohari ya dawa za kanda kama si hivyo kuna tatizo na inawezekana MSD mnashirikiana na hawa"

Vile vile Naibu Waziri huyo ameitaka MSD kufanya ziara kwenye vituo vya umma mara kwa mara

Akisoma ripoti ya afya kwa Wilaya ya Mpwapwa Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Said Mawji alisema hali ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya huduma ni asilimia 69 na kwa hospitali ni asilimia 90.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi