Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Miaka 3 ya JPM Imechagiza Mageuzi Katika Sekta ya Anga
Nov 23, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_38716" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum katika kipindi cha MORNING TALK cha Ebony Fm Mkoani Iringa kuhusu Utekelezaji wa Serikali katika Kipindi cha Miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli[/caption] Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ndani ya miaka mitatu imeweza kuleta ukombozi katika sekta ya anga kwa lengo la kuchagiza mageuzi katika sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa kipindi cha Morning Talk cha redio Ebony Fm Mjini Iringa.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli amekuwa akitekeleza yale yote aliyoyaahidi ambapo mpaka sasa anaendelea kutekeleza aliyoyaahidi katika sekta ya anga.

"Mpaka sasa nchi yetu inandege tatu aina ya Bombadia na Dreamliner moja na pia mwezi Desemba tunaleta AIRBUS mbili ili kuendeleza na kuchagiza mageuzi katika sekta ya Anga" amefafanua Dkt. Abbasi.

Aidha, Dkt. Abbasi anaongeza kuwa "Leo hii Shirika letu la ndege limeongeza idadi ya abiria wanaotumia usafiri huo kwa mwezi kutoka 4000 hadi kufikia 36000".

Akizungumzia kuhusu Ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea, Dkt Abbasi amesema kuwa, kufikia mwaka 2019 Desemba kipande cha reli cha kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kitakuwa kimekamilika na treni ya kwanza ya umeme itatoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Vile vile Dkt. Abbasi amebainisha kuwa Serikali imeanzisha mfumo wa kuleta mbolea na baadhi ya pembejeo kwa pamoja ili kuweza kusaidia kupunguza gharama na kusaidia maendeleo katika sekta ya kilimo.

"Wakulima waendelee kufanya kazi katika maeneo yako kwani Serikali inafanyia kazi changamoto zote ikiwamo ya masoko kwa lengo la kusaidia maendeleo katika sekta hiyo muhimu kwa Watanzania" ameongeza Dkt. Abbasi.

Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesema kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua kubwa ya kujenga nchi kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mbali mbali mikubwa ya maendeleo ikiwemo Mradi wa Kamuzalisha Umeme wa Stieglers.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi