Mhe. Rais Samia Akutana na Ujumbe Maalum wa Mfalme wa Saud Arabia, Azindua mradi wa maji Chalinze, Pwani
Mar 22, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudia Arabia, Mhe. Ahmed Abdulazizi Kattan mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoa Kitambaa kuzindua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga katika tukio lililofanyika Chalinze mkoani Pwani leo tarehe 22 Machi 2022.
Mtambo Mpya wa Maji Mlandizi-Chalinze-Mboga.
Wananchi wa Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga katika tukio lililofanyika Chalinze mkoani Pwani leo tarehe 22 Machi 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Chalinze mkoani Pwani katika Mkutano uliofanyika Viwanja vya Polisi Chalinze mkoani Pwani mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga leo tarehe 22 Machi 2022.