Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhe. Dkt. Mpango Azindua Kitabu cha Historia ya Muungano
Apr 26, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff – MAELEZO

Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua kitabu cha historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kinacholenga kuongeza uelewa kuhusu Muungano huo.

Andiko hilo linaloitwa “Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Chimbuko, Misingi na Maendeleo” limezinduliwa leo jijini Dodoma katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete.

“Kitabu kinaeleza chimbuko la historia na misingi iliyowezesha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kufanyika, kuimarika na kudumu kwa miaka 58 sasa na jinsi Waasisi wa Muungano walivyokuwa viongozi wa mfano waliotanguliza masalahi ya Taifa mbele kuliko maslahi yao binafsi.

“Aidha kitabu hicho kimebainisha mafanikio yaliyopatikana kwa miaka 58 ya muungano pamoja na hoja za muungano zilizojitokeza na hatua zilizochukuliwa kuzipatia ufumbuzi,” amearifu Makamu wa Rais.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema kero 18 kati ya 25 za Muungano zimepatiwa ufumbuzi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi