[caption id="attachment_37333" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurungezi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la UNICEF, Nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Leila Pakkala alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Dodoma, Oktoba 24, 2018.[/caption]
Na: Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ameiomba UNICEF kuunga mkono jitihada za Serikali katika programu ya ukuzaji ujuzi nchini inayolenga kuwawezesha vijana kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri.
Mhe. Mhagama ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokutana na Mkurugenzi wa UNICEF nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Leila Pakkala.
[caption id="attachment_37334" align="aligncenter" width="822"]"Ninaomba UNICEF izidi kunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika masuala yanayowahusu vijana na watoto ili tuandae kizazi hiki kwa majukumu makubwa ya kitaifa, kwani hawa ndio taifa la kesho" alisema Mhagama
Waziri Mhagama ameishukuru UNICEF kwa kushirikiana na Serikali katika kushughulikia kwa pamoja masuala ya Afya, Elimu, mapambano dhidi Ukimwi na ajira za utotoni.
[caption id="attachment_37336" align="aligncenter" width="900"]Kwa upande wake, Mkurungezi Mkazi wa UNICEF Nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Leila Pakkala amesema kuwa Shirika hilo lina mipango mbalimbali inayolenga kuwainua vijana katika sekta mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza kuwa vijana ndio tegemeo la taifa, hivyo UNICEF itaendeleza ushirikiano na Serikali katika kutekeleza mipango yake.
"Ninaipongeza Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza katika kukuza uhamasishaji kwa vijana na kuwashirikisha kwenye masuala ya kimaendeleo" alisema Bi. Pakkala
UNICEF imekuwa ikishirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi na programu za Kitaifa juu ya masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ambayo yameleta manufaa katika nchi.