Na Oscar Assenga, Tanga.
Bandari ya Tanga inatarajiwa kuanza kupokea Meli za Magari ifikapo Mwezi Mei mwaka huu ambayo yatakuwa yakipelekwa kuhifadhiwa eneo la Mwambani Jijini Tanga.
Hatua hiyo inatajwa kwamba itafungua fursa mpya za kiuchumi kwenye Bandari ambayo kwa sasa inafanyiwa maboresho makubwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake.
Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Mrisha Masoud wakati wa ziara ya wadau wa Bandari ya Tanga walipotembelea bandarini baada ya kumalizika kwa kikao chao na mamlaka hiyo.
Meneja Mrisha alisema eneo la mwambani lina ukubwa wa hekta 176 sasa kama walivyosema wanatarajia kuhudumia shehena kubwa kutoka 750,000 mpaka kufikia Milioni 3000,000 hivyo mzigo utakuwa ni mwingi.
Alisema kutokana na hilo wamependelea eneo hilo kulitumia kufanya shughuli za nyingine ikiwemo kupakilia mizigo kwenye makontena na kuweka kontena tupu na shughuli zinazoambatana na shughuli za kibandari.
Hata hivyo aliwaeleza wadau hao kuhusu maboresho ya Bandari ya Tanga ikiwemo jinsi mradi wa maboresho ulivyo mpaka sasa awamu zote tatu ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni kuongeza kina kutoka mita tatu mpaka mita 13 kwenye mlango bahari, sehemu ya kugeuzia meli na vifaa ambapo iligharimu shilingi bilioni 172.3.
Alisema pia wameona maboresho ya bezi mbili zenye urefu mita 450 zilizogharimu Bilioni 256.8 na wameona ahadi iliyotolewa na mkandarasi ambapo mpaka mwezi Mei watakabidhiwa kipande cha mita 150 na itakapofika Oktoba wakabidhi mita zote 450.
Hata hivyo alisema kwamba hoja ambazo zimewasilishwa na wadau kwenye kikao hivyo wamezichukua na kwenda kuzifanyia kazi na wao wametusikiliza kuwaeleza namna maboresho makubwa yaliyofanyika na kuahidi kuitumia kwa ajili ya kupitisha shehena zao.
Awali akizungumza mara baada ya ziara ya wadau hao kwenye Bandari hiyo kushuhudia maboresho makubwa yaliyofanyika, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu, Nikodemas Mushi alisema mkutano huo ulikuwa na nia ya kukutana na wadau wanaohudumiwa na Bandari ya Tanga ambayo inayohudumia Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo nchi jirani Rwanda.
Alisema kupitia mkutano huo wanaamini watafungua ukurasa mpya wa kibiashara na lengo lao ni kuondoa nafasi ya maswali na hoja na changamoto mbalimbali ambazo hazijaweza kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa Masoko na Uhusiano alisema wadau wametoa maoni huku akieleza kwamba Meneja wa Tanga na timu yake wamesikia na wamejipanga tayari kuanza kuzifanyia kazi mara moja.
Alisema na suala ambalo linawahusu makao makuu watalibeba na kulipeleka huku ili yaweze kufanyiwa maamuzi na huo ni mkakati wa kimasoko