Na Ahmed Sagaff – MAELEZO
Wakazi wa Jiji la Mbeya wamefanya matembezi ya amani kwa lengo la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na faida ya kazi zake ambazo zimewapa unafuu wa maisha wakazi wa jiji hilo.
Akizungumza katika shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera amearifu kuwa Rais Samia ametoa zaidi ya shilingi bilioni 22 kwa ajili ya sekta ya afya jijini humo ambazo zimejenga hospitali na vituo vya afya sambamba na kununua vifaa tiba.
Aidha, Mhe. Homera amesema Rais Samia ametoa Shilingi bilioni 64.8 kwa sekta ya elimu, Shilingi bilioni 19 katika sekta ya maji na zaidi ya Shilingi bilioni 119 kwa sekta ya miundombinu.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Dkt. Angelina Lutambi amesema watu wa Mbeya wanatambua hatua ya uimarishaji wa huduma muhimu zinazotolewa na Serikali jijini humo.
“Kuna mambo mengi sana ambayo Mheshimiwa Rais amewafanyia wana Mbeya,” amearifu Dkt. Lutambi.