Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Mbalimbali ya Msiba wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika Picha
Mar 01, 2024
Matukio Mbalimbali ya Msiba wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika Picha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo alipohani msiba wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Machi 01, 2024 Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Na Idara ya Habari - Maelezo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipohani msiba wa baba yake ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Machi 01, 2024 Mikocheni ji jini Dar es Salaam.

 


Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo alipohani msiba wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Machi 01, 2024 Mikocheni jijini Dar es Salaam.

 

Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akimpa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipohani msiba wa baba yake ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Machi 01, 2024 Mikocheni ji jini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akitoa pole kwa Mama Sitti Mwinyi na Mama Khadija Mwinyi kufuatia kifo cha Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kilichotokea jana tarehe: 29 Februari, 2024 Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi (kulia) amefika nyumbani kwa Hayati Mzee Mwinyi kuwafariji Mama Sitti Mwinyi na Mama Khadija Mwinyi kufuatia kifo cha Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kilichotokea jana tarehe: 29 Februari, 2024 Dar es Salaam.

 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz akiteta na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi katika msiba wa Hayati Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Msafara uliobeba mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi ukielekea katika msikiti wa BAKWATA Kinondoni kwa ajili ya taratibu za kidini leo Machi 1, 2024.

 

Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi ukiingizwa katika msikiti wa BAKWATA Kinondoni kwa ajili ya taratibu za kidini leo Machi 1, 2024.
Viongozi wa dini wakimswalia Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi