Mrasimu ramani Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi akieleza kwa waandishi wa habari faida za kutumia mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
Mtaalamu wa masuala ya Jiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi Matha Macha akitoa maelezo kuhusu namna mfumo huo unavyofanya kazi.
Mrasimu ramani msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Rahim Mussa akisisitiza kuhusu namna mfumo huo unavyochochea maendeleo na kusaidia Serikali kuokoa gharama kubwa zilizokuwa zikitumika awali katika kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali.
Mrasimu ramani Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi (wapili kutoka kushoto) akiongoza ujumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutembelea kijiji cha Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo ujumbe huo umeambatana na waandishi wa habari kujionea mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
Mwenyekiti wa kijiji cha Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo ni ujumbe wa NBS na waandishi wa habari walitembelea kujionea jinsi mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia unavyofanya kazi na jinsi ulivyounganishwa na Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu , hiyo ilikuwa wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo za tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
(Picha zote na Frank Mvungi)