Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Ziara ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Visiwani Zanzibar
Feb 09, 2021
Na Msemaji Mkuu

Katibu Mkuu Wizara ya  Ardhi  na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanibar (SMZ) Bw. John Kilangi akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuhamasisha wananchi kurasimisha ardhi ili kuondoa migogoro na kuwawezesha kutumia hatimilki kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuvutia uwekezaji.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya  Ardhi  na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanibar (SMZ) Bw. John Kilangi na watumishi wa Wizara hiyo  wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Ofisi za Wizara hiyo leo Februari 9, 2021.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akieleza jambo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango huo  walipotembelea Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) leo Februari 9, 2021.

Afisa Mrasimishaji wa ardhi Unguja Zanzibar  Bi. Shawana Soud  Khamis akiwasilisha mada kwa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Wizara ya  Ardhi  na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Mrajis wa ardhi Dkt. Abdul- Nasser  Mikmany akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) leo Februari 9, 2021 wakati wa ziara ya Kamati hiyo visiwani Zanzibar kujionea hatua iliyofikiwa katika urasimishaji ardhi na biashara.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wakifuatilia  hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya  Ardhi  na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanibar (SMZ) Bw. John Kilangi wakati walipomtembelea Ofisini kwake Maisara Unguja.

(Picha zote na MAELEZO)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi