Matukio katika Picha: Waziri Mkuu Majaliwa Akiwa Bungeni. Azungumza na Balozi wa Indonesia Nchini Ofisini Kwake
Jun 06, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, bungeni jijini Dodoma, Juni 6, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, bungeni jijini Dodoma, Juni 6, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Tri Yogo Jatmiko ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma Juni 6, 2022 kujitambulisha baada ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Januari 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Tri Yogo ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma Juni 6, 2022 kujitambulisha baada ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Januari 2022.