Matukio katika Picha: Waziri Bashungwa Afunga Kikao Kazi cha Maafisa Habari/Mawasiliano Serikalini
May 13, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali ( TAGCO ), Paschal Shelutete akimkabidhi shati la Chama hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa mara baada ya Waziri huyo kufunga kikao kazi cha Maafisa hao Jijini Tanga leo tarehe 13 Mei 2022.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akitoa salamu fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kufunga Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachofanyikia Jijini Tanga leo tarehe 13 Mei 2022.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitoa neno la utangulizi wakati wa ufungaji wa Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachofanyakia Jijini Tanga leo tarehe 13 Mei 2022.
Maafisa wa Habari/Mawasiliano wakiwa katika kilele cha Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali ambapo Maafisa hao wamepata nafasi ya kuangalia filamu ya Tanzania ‘The Royal Tour’ leo Mei 13, 2022.