Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Ujenzi wa Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma
Jan 07, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39539" align="aligncenter" width="900"] Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , jengo hilo linajengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_39545" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma kama walivyokutwa mwishoni mwa wiki.[/caption] [caption id="attachment_39540" align="aligncenter" width="900"] Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_39541" align="aligncenter" width="900"] Hatua iliyofikiwa katika jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kama inavyoonekana katika picha kwenye mji wa Serikali Ihumwa ambapo ujenzi unaendelea, hayo yamejiri mwishoni mwa wiki wakati Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe (hayupo pichani) na ujumbe wake walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo.[/caption] [caption id="attachment_39542" align="aligncenter" width="900"] Muonekano wa jengo la Wizara ya Katiba na Sheria katika mji wa Serikali Ihumwa ambapo ujenzi wa majengo ya Wizara zote unaendelea.[/caption] [caption id="attachment_39543" align="aligncenter" width="900"] Muonekano wa jengo la Wizara ya Maji katika mji wa Serikali ambapo ujenzi wake unaendelea kama ilivyokutwa mwishoni mwa wiki.[/caption] (Picha zote na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi