Matukio katika Picha: Rais wa CAF Atembelea Uwanja wa Mkapa
Feb 13, 2026
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe amefanya ziara katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambao ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika katika AFCON 2027.
Katika ziara hiyo, iliyofanyika Februari 13, 2026 Dkt. Motsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda ambapo, Mhe. Makonda alieleza kuwa, maendeleo ya uwanja huo ni kutokana na kazi nzuri ya uwekezaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Na
Mwandishi Wetu