Matukio katika Picha: Muendelezo wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari/Mawasiliano Mkoani Tanga
May 10, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa (aliyesimama) akizungumza na Maafisa Habari/Mawasiliano (hawapo pichani) katika siku ya pili ya kikao kazi hicho kinachoendelea jijini Tanga.
Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Kassim Nyaki akichangia hoja katika kikao kazi cha Maafisa hao kinachoendelea jijini Tanga.
Baadhi ya Maafisa Habari/Mawasiliano wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao kazi cha Maafisa hao kinachoendelea jijini Tanga.
Baadhi ya Maafisa Habari/Mawasiliano wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao kazi cha Maafisa hao kinachoendelea jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akiwa na Maafisa Habari/ Mawasiliano wa Serikali leo Mei 10, 2022 wakati walipotembelea Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Tanga kwa lengo la kujionea maendeleo ya upanuzi huo.
Maafisa Habari/ Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika ziara kutembelea Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Tanga kwa lengo la kujionea maendeleo ya upanuzi huo.
Wafanyakazi wakiendelea na kazi katika Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Tanga leo Mei 10, 2022