Matukio katika Picha: Msemaji Mkuu wa Serikali Azindua Studio za BBC kwa Ofisi za Tanzania
Mar 08, 2024
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi, leo Machi 8, 2024 amemuwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye katika uzinduzi wa studio za kidijitali za Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwa ofisi za Tanzania uliofanyika katika ofisi zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam.
Na
Paschal Dotto-Maelezo