Matukio katika Picha: Mazingira ya Wakazi Wapya Msomera
Jun 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Muonekano wa Shule mpya ya Sekondari Msomera iliyopo kijiji cha Msomera, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Msomera ni makao mapya kwa wakazi wanaohama kutoka eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Nyumba za makazi ya wananchi wapya ambao wameamua kuondoka kwa hiyari katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha na kuhamia katika kijiji cha Msomera, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Muonekano wa moja ya eneo la kuogesha wanyama (josho) lililopo kijijini Msomera, wilayani Handeni, Mkoani Tanga.
Mkazi mpya akichunga wanyama sehemu ambayo ina uhakika wa maji na chakula kwa wanyama kwenye makazi yao mapya kijijini Msomera, wilayani Handeni, mkoani Tanga.